VIWANGO VYA FIFA

>>>KUMI BORA, Colombia yatinga, yapanda Nafasi 13!!
>>>BRAZIL Washuka 2, Wapo wa 14!!
FIFA_LOGO_BESTSpain, ambao ndio Mabingwa wa Ulaya na Dunia, wameendelea kushika Nambari Wani kwenye Listi ya FIFA/Coca Cola ya Ubora Duniani iliyotolewa leo huku Tanzania ikibakia Nambari 132 na kwenye Kumi Bora Portugal imepanda na kushika Namba 3, England imeporomoka na sasa ipo nafasi ya 5 kutoka Namba 3.
Barani Afrika Ivory Coast ndio wapo juu na wapo nafasi ya 16 ambayo ni ile ile kama ilivyokuwa Mwezi uliopita.
Colombia wameingia Kumi Bora baada ya kupanda nafasi 13 huku Denmark na Croatia zikiporomoka kutoka Kumi Bora.
Brazil, Mabingwa wa Dunia mara 5, wameporomoka nafasi mbili na sasa wapo nafasi ya 14.
Listi nyingine mpya itatolewa Novemba 7.
KUMI BORA:
1 Spain
2 Germany
3 Portugal
4 Argentina
5 England
6 Netherlands
7 Uruguay
8 Italy
9 Colombia
10 Greece